KATIBU Mkuu wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), DK. Wilbroad Slaa amesema hakuwa likizo ila
aliamua kuachana na siasa baada ya kutokubaliana na maamuzi ya chama chake
yaliyotokea Julai 28,2015 saa 3 usiku.
Wanahabari wa Kampuni ya
Global Publishers wakiwa ofisini kwao, Bamaga, Mwenge wakifuatilia hotuba ya
Dk. Slaa iliyokuwa ikifanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar.
Asema lazima ajitokeze kusema na kuweka ukweli
hadharani
Asema sina tabia ya kuchengachenga nasimamia
ninachokiamini Mengi yamesemwa na kuandikwa magazetini
Sina ugomvi na kiongozi yoyote, maana siasa si ugomvi, sina chuki, sina hasira
na mtu yeyote
Siasa inayoongozwa na propaganda, ulaghai ni kuleta vurugu katika taifa na
nimekataa hayo yote.Ni kweli nilishiriki katika majadiliano tangu mwanzo
Misingi niliyoweka ni kwamba
Lowassa atangaze kuwa ameachana na chama chake na aeleze anakwenda chama gani
kwanza na ajisafishe na tuhuma zake
Asema hawezi kumsafisha mtu bila
yeye kufanya hivyo
Asema alihoji kama Lowassa anakuja
Chadema kama faida au mzigo (assets au liability)
Asema anataka mgombea mwenye
uwezo, sifa na kuiongoza Chadema kuiondoa CCM.
Kama ni assets anakuja na akina
nani? vijana wa mitaani, bodaboda au watu wa aina gani? ni viongozi makini?
Asema aliambiwa kuwa anahama na
wabunge 50, wenyeviti wa mikoa 22, wenyeviti wa CCM wilaya 82.
Sikupewa majina ya wabunge wala
wenyeviti.
Nikatakiwa kuitisha kikao nikaitisha lakini sikuwa na majibu kama Lowassa
ni Assets au Liability. Tangu 2004
sikuwahi kutofautina na mwenyekiti wangu bali tulitofautia kwa hilo
Asema aliandika barua ya kujiuzulu
kwa M/kiti Prof. Safari barua ikachanwa.
Siasa ni sayansi haitaki uongo
wala ulaghai au propaganda Asema mke wake halipwi chochote kutoka Chadema na
amekuwa akizunguka nchini kwa mshahara wa Dk. Slaa.
0 comments:
Post a Comment