umojannguvu.blogspot.com

Tuesday, 1 September 2015

Maswali kwa mhe: Edward Lowassa



MASWALI KWA MHE. EDWARD LOWASSA

Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph MungaiJoseph Mungai akihutubia mkutano wa UKAWA Mafinga
Bwana Luke kama hutajali naomba ubandike haya mawazo yangu.
jina langu ni Tom

Nimesoma katika gazeti la mwananchi la leo ambalo lili mnukuu mgombea urais kupitia Ukawa Ndugu Edward Lowassa alipokuwa akihutubia huko Iringa akiwaahidi watanzania elimu ya bure kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu kuanzia January mwakani 2016. Zaidi aliahidi kulipa madai yote ya Walimu na wafanyakazi wengine wa serikali ambapo haya ni mabilioni ya pesa. Huyu mgombea hakufafanua bayana ni njia zipi zitatumika au vyanzo gani vya pesa vya kugharimia yote haya kwa miezi michache iliyobaki kufika January 2016.

Mimi si mshahabiki wa chama chochote ( independent) bali ninapo sikia ahadi ambazo naziona kama haziwezekani kutimizwa hasa ukizingatia muda uliotajwa na huyu mheshimiwa inasikitisha. Naelewa kwamba nia yake ni kuwa rais, sina tatizo na hilo lakini hili la kuahidi elimu bure kuanzia January mwakani linatia shaka. Labda lengo ni kupata kura za wanafunzi na walimu, sina uhakika. Najua kuna nchi ambazo zinatoa elimu ya bure lakini uchunguze hizi nchi zimeanzia wapi na vyanzo vyake vya mapato ya kugharimia elimu ya bure vinatoka wapi. Hata nchi tajiri kama Marekani ukiacha elimu ya msingi elimu siyo bure.

Baadhi ya hizi nchi wananchi wake hutozwa kodi kubwa sana kitu ambacho ni kama haiwezakani kwa Tanzania kwani ajira zenyewe bado ni shida na kilimo ndiyo hivyo tena. Wakati huohuo huyu mheshimiwa anasema ataondoa ushuru wa mazao. ( Hii si ndiyo kodi yenyewe?)

Maoni yangu ni kwamba hawa wagombea ni ama wanajua au wanadhani kuwa uwezo wa watanzania wengi kuelewa mambo au takwimu bado ni mdogo sana ( so they can get away with it) na hii imekuwa kama utamaduni kwamba waambie wanachotaka kusikia nipate ninachotaka mambo mengine baadae.

Juzi hapa Lowassa aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi uwanja wa jangwani kumsikiliza akiahidi kwamba kuna vigogo wengi wa CCM wangejiunga na UKAWA. Labda kama nilipitwa lakini sijasikia hao vigogo wengine wakijiunga na UKAWA angalau siku hiyo ya ufunguzi. Ni jambo dogo lakini kwa mgombea urais inashusha credibility.

Ujumbe kwa wagombea wote, Achaneni na kuongea na watanzania kama mnaongea na watoto. Na watanzania tusishabikie tu bali tuwabane hawa wanaotaka kuwa viongozi wetu kulingana na ahadi ambazo nyingi zinaonekana kama ni hewa. Awe ni mgombea wa ccm au ukawa nk, watwambie ukweli siyo longolongo. Longolongo imepitwa na wakati.
MASWALI KWA MZEE LOWASA ambayo niliyapata jamii forums
1. Gazeti la Raia Mwema la Novemba 2010 liliripoti na kuonesha picha ya nyumba ambayo familia yako inamiliki Uingereza. Ukasema ni ya mwanao, je kwa nchi masikini kama ya kwetu, ni sahihi kwa kiongozi wa UMMA kumiliki nyumba kubwa ya kifahari nje ya nchi?
2. Mkapa alipounda baraza jipya la mawaziri mwaka 1995 alikuacha, wengi wanasema kuwa Nyerere alimuambia asikupe hata uwaziri, Je kwanini Mwalimu alikukataa?
3. Tangu mwaka 1994, zaidi ya miaka ishirini sasa (20 years), Afrika kusini imekuwa ikikodisha nyumba yako masaki kama ubalozi wake, kuna tetesi kwamba huko nyuma walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu, na kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhama lakini wanatishiwa. Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa zaidi ya miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo? Je kiasi hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?
4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya ,masaki ambayo mzee mandela alikuja mwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya wa afrika kusini ndicho chanzo kikuu cha mwalimu kusema inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi wa umma maisha yake yote na mshahara wake unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena kukodishwa na serikali ya kigeni? unasemaje kuhusu hili?
5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule mzeri handeni, ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya taifa, lakini ukajimegea na ukamega maeneo mengi zaidi. Ranchi iyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa Umma, Je, mtu aliyewahi kuwa waziri wa mifugo na waziri mkuu, kujiuzia ranchi iliyokuwa ya serikali, inaendana na dhana ya uongozi uliotukuka??? Tukikupa madaraka makubwa zaidi, hautajiuzia kila kitu?
Vilevile, katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki ardhi, Je, kiongozi kuhodhi eneo kubwa la ardhi, inatupa picha gani wananchi?
6. Kwenye sakata la Richmond, ujasiri nikusema ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema ukweli na usingejiuzulu kwenye richmond, chama kingeathirika vipi wakati unasema hakuna kosa lililoanyika?
7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa, ukisimama tu karibu na kikwete, unahangaika kutuma picha kwenye magazeti na mitandao yote?
8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa Umma, una lipi jipya ambalo umelisahau, na sasa utalifanya katika huu urais wako unaougharamia kwa pesa nyingi?
9. Umekuwa waziri wa ardhi, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa maji, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa mazingira, mbona kuna matatizo ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira? Umekuwa waziri wa mifugo, mbona wafugaji bado masikini, na wanahangaika? Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda?
10. Umetoa mchango gani kwenye bunge maalum la katiba katika kuyatetea maoni ya wananchi, hali ulikuwa ukishuhudia yakipotoshwa na chama chako?

0 comments:

Post a Comment

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

CHAT BOX

Post zilizo tumwa

Recent Posts Widget

Tangaza Biashara yako mtandaoni

TANGAZA BIASHARA NAMI HAPA KWA BEI NAFUU KABISA

Unaweza kutangaza biashara yako sasa na hlmservice pia uta pata kujua mambo mengi ambayo mbali na biashara yako unaweza ukatengeneza pesa kwa namna moja ama nyingine kama jinsi nilivo elezea katika Makala za nyuma hapo

Wafanya biashara wengi wanatumia mda mwingi namna gani ya kukuza biashara zao ,Ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unahitaji kuitangaza biashara yako ili kuwa na mtandao mkubwa na wateja wako ,ni vyema ukatangaza biashara yako katika mitandao ili bidhaa zako zijulikane kwa haraka na upesi .

Pia wewe mfanya biashara ukiitaji kuwa na blog yako wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini , bei ni nafuu kabisa

Pia ukiitaji kuitangaza biashara yako kupitia blog yangu bei ni ndogo kabisa huu ni wakati wako wewe mfanya biashara

+255758061575 & +255684860817

henrylameck@gmail.com

henrylameck90@yahoo.com

Tukuyu Tour & Safari

Vadacom Ni Zaidi

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Kilimo Kwanza

Hlm servise

Latest movie

Movies

Computer books

Computer books