umojannguvu.blogspot.com

Sunday 23 August 2015

KAMPENI ZA URAIS ZAANZA RASMI TUME YATOA RATIBA ZA MAENEO NA MUDA WA KAMPENI



KAMPENI ZA URAIS ZAANZA RASMI TUME YATOA RATIBA ZA MAENEO NA MUDA WA KAMPENI



Tume ya Taifa ya uchaguzi inakutana na Kamati Maalumu inayo undwa na wajumbe kutoka vyama nane vilivyo na wagombea wa urais na makamo kuandaa Ratiba ya mikutano ya hadhara kurahisisha kubaini vyama vilivyopanga mkutano mmoja katika mkoa mmoja, wilaya moja, na Eneo moja kwa Tarehe moja,Mkurugenzi wa NEC Kailima Ramadhani amesema anafarijika sana na ushirikiano wanaouonyesha Wawakilishi Wa vyama katika kuhakikisha mchakato kuwa wa Amani na utulivu bila kujali itikadi za vyama vyao kikao kitaendelea kutwa nzima ya leo hadi kufikia makubaliano ya Ratiba kwa vyama vyote.

https://www.facebook.com/TumeyaTaifayaUchaguziTanzania
+255(0)772 55 55 53
LISTEN LIVE
http://myradiostream.com/focusradiotz
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
YOUTUBE / TV
http://bitly.com/1Leujup
VIPINDI VYA REDIO
http://bitly.com/1Clt0r8
FACEBOOK
http://bitly.com/1zIiIkq
TWITTER
http://bit.ly/1678Vq2(P.T)


Wahamiaji 2000 waokolewa Mediterranea

Walinzi wa pwani wa Utaliano wanasema kuwa waliaongoza shughuli za kuwaokoa wahamiaji 2,000 hivi ambao walituma ishara ya kuwa taabani kwenye mashua nje ya pwani ya Libya. Mashua kadha zinashiriki katika uokozi.



Bahari baina ya Libya na Utaliano, ndio njia inayotumiwa kwa muda mrefu, na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ili kuingia Ulaya.



Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja wa mataifa unasema kuwa bahari ya Mediterranea ndio kivukio maarufu.

Kufikia sasa takriban watu laki moja wamewasili katika ufukwe wa Italia .




Wengine zaidi ya laki moja u nusu 160,000 waliwasili Ugiriki.

Jarida moja la Norway Aftenposten, limesema kuwa manuari ya kijeshi ya taifa hilo Siem Pilot, liko njiani kuwasaidia wahamiaji hao walioko mashakani.

Manuari hiyo iliwaokoa wahamiaji 320 mapema leo kabla ya kurejeshwa tena huko huko kushiriki operesheni hii ya kuoko nafsi za watu wanaokisiwa kuwa takriban 3,000

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemsuta kiongozi wa upinzani wa Kenya, Raila Odinga, kwa kupinga mkataba wa uuzaji wa sukari uliotiwa sahihi majuzi.





Museveni alisema kuwa Odinga hafaaamu anachokisema.

''hata ndugu yangu odinga anazungumzia maswala ya sukari,bila kufahamu ukweli wa maswala hayo'' Museveni.

Kenya imekuwa ikizuia sukari yetu na mahindi ilihali Uganda imekuwa ikiagiza bidhaa za thamani kubwa pasi na kujali kuwa inawasaidia kujiendeleza.

''Wewe ni mkurugenzi wa kampuni ilihali kazi yako kubwa ni kuzuia sukari ya Uganda isiingie Kenya.

 

Hii ni akiligani jamani ?''aliuliza Museveni.

'Nafikiri nitampigia Raila simu nimwambie kuwa sukari ya Uganda itaingia Kenya sawa na vile mali ya Kenya inaingia Uganda bila vizingiti' aliongezea Museveni.

Rais Museveni aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wageni waalikwa na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki lililoanza vikao vyake jiji Kampala Uganda.

Museveni alisema mataifa wanachama wa muungano wa kanda hii ya Afrika Mashariki na kati sharti yafuate kanuni za muungano ikiwemo Kenya.

 

''Kenya inasafirisha mali ya thamani ya dola milioni 700 kuingia Uganda na kununua bidhaa zenye thamani ya dola milioni 150 kutoka Uganda, Ninamshukuru rais Kenyatta kwa kuondoa mashrti makali na vizuizi vilivyokuwa vinakataza bidhaa za Uganda Kuingia Kenya.alisema Museveni.
Uganda kwa sasa inasaga sukari tani 450,000 huku ikitumia takriban tani 320,000 na hivyo inasalia takriban tani 145,000 za sukari.

Hii ndiyo sukari ambayo sasa itaruhusiwa kuuzwa nchini Kenya.
Kwa Upande wake Kenya inazalisha takriban tani 600,000 ya sukari huku ikihitaji kati ya tani 800,000 na 850,000 kwa hivyo inanakisi ya takriban tani 250,000 za sukari kukidhi mahitaji ya raia wake.


Bwana Odinga amekuwa akidai kuwa sukari iliyokubalika kuingia Kenya kutoka Uganda sio sukari inayoundwa nchini humo bali ni sukari inayotokea Brazil na kupakiwa katika magunia ya sukari ya makampuni ya kusaga sukari ya uganda kwa minajili ya kukwepa kulipa kodi.

Wazo hilo limepuziliwa mbali na serikali ya Kenya ambayo imekuwa ikisisitiza kuwa sukari ya Uganda itaendelea kuingia Kenya chini ya mpango wa jumuia ya Afrika Mashariki COMESA.

Iran na Uingereza kufungua balozi zao

Uingereza na Iran zinatarajiwa kufungua balozi kwenye miji yao mikuu licha ya kuwepo uhusiano mbaya katika ya Iran na nchi za magharibi.




Waziri wa mashauri ya kigeni wa Iran Philip Hammond anatarajiwa kuwasili mjini Tehran kwa sherehe hizo.

Atakuwa afisa wa kwanza wa ngazi ya juu zaidi wa Uingereza kuzuru Iran tangu miaka 12 iliyopita.

Ubalozi wa uingereza ulifungwa mwaka 2011 wakati ulisakwa na waandamanaji.

Makubaliano ya nyukia ya mwezi uliopita kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani yametoa njia ya kuboreshwa kwa uhusiano kati yao.Taarifa toka bbc leo

Saturday 22 August 2015

Mkuu wa mkoa wa mbeya Abbas Kandoro asisitiza wanainchi kuwa makini




Mkuu wa mkoa wa mbeya Abbas Kandoro amesisitiza wananchi kuepuka kuwa chanzo cha kuvuruga amani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi

Amesisitiza wanainchi kusikiliza kwa makini sera za wagombea wao ili kuweza kuchagua kiongozi bora na sio kiongozi mwenye tamaa na madaraka tu.

Sumaye kutimkia Chadema leo tazama matukio katika picha hapa




Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kulia), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe Dar es Salaam leo mchana, baada ya kujiunga na chama hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho
 









 Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kushoto) Akizungumza jambo
 




Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

CHAT BOX

Post zilizo tumwa

Recent Posts Widget

Tangaza Biashara yako mtandaoni

TANGAZA BIASHARA NAMI HAPA KWA BEI NAFUU KABISA

Unaweza kutangaza biashara yako sasa na hlmservice pia uta pata kujua mambo mengi ambayo mbali na biashara yako unaweza ukatengeneza pesa kwa namna moja ama nyingine kama jinsi nilivo elezea katika Makala za nyuma hapo

Wafanya biashara wengi wanatumia mda mwingi namna gani ya kukuza biashara zao ,Ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unahitaji kuitangaza biashara yako ili kuwa na mtandao mkubwa na wateja wako ,ni vyema ukatangaza biashara yako katika mitandao ili bidhaa zako zijulikane kwa haraka na upesi .

Pia wewe mfanya biashara ukiitaji kuwa na blog yako wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini , bei ni nafuu kabisa

Pia ukiitaji kuitangaza biashara yako kupitia blog yangu bei ni ndogo kabisa huu ni wakati wako wewe mfanya biashara

+255758061575 & +255684860817

henrylameck@gmail.com

henrylameck90@yahoo.com

Tukuyu Tour & Safari

Vadacom Ni Zaidi

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Kilimo Kwanza

Hlm servise

Latest movie

Movies

Computer books

Computer books