umojannguvu.blogspot.com

Tuesday 8 September 2015

Lowassa: Msikose usingizi


MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameisimamisha tena Dar es Salaam kwa saa kadhaa huku akiwataka Watanzania kutokosa usingizi kwani hakuna kura itakayoibwa.
Lowassa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti alipokuwa kwenye mikutano ya kampeni Wilaya ya Kinondoni katika majimbo ya Kawe na Kibamba.
Akiwa katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi, Bunju A kwenye Jimbo la Kawe, alisema watu wasikose usingizi bali wasubiri Oktoba 25 ifike.
Licha ya kwamba Lowassa alifika Bunju saa saa 9:25 alasiri, viwanja hivyo vilianza kufurika watu kuanzia asubuhi kwani mkutano ulitarajiwa kuanza saa 5:00 asubuhi.
Hali ilikuwa hivyohivyo kwenye Jimbo la Kibamba ambako licha ya kiongozi huyo kufika katika eneo hilo saa 11:30 jioni, watu walianza kufurika asubuhi, hali iliyofanya barabara ya Morogoro kupitika kwa shida.
MSIKOSE USINGIZI
Akizungumza katika Mkutano wa Kawe, Lowassa alisema shaka dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), iliyopo sasa inatokana na jeuri ya wapinzani wao.
“Kuna maneno mengi yanasemwa kuhusu NEC... nawahakikishieni hawataiba ng’o, tuko imara, tutalinda kura zetu hadi zitakapohesabiwa.
“NEC na CCM hamtaweza kuiba kura zetu, Watanzania tukatae kuibiwa kura na kulaghaiwa,” alisema Lowassa.
Aidha Lowassa alisema kuna watu wa ofisini wanataka mageuzi, lakini wanatishwa, na wengine ni wafanyabiashara wanaotaka kutusaidia.
“Hao wanaowatisha walie tu, hawawezi kumshughulikia mtu yeyote,” alisema.
Alisema atabadilisha mfumo wa utendaji kazi wa Serikali kutoka ulivyo sasa na kuwa wa kasi. “Itakuwa ni spidi 120”, alisema.
Aliendelea kusema: “Zimebaki siku 48, tukatae msongamano wa magari Dar es Salaam, adha na tabu katika hospitali na vituo vyetu vya afya, michango ya shule za sekondari na msingi, tatizo la maji na ajira.
“Fanyeni uamuzi mgumu tuibadilishe wizara ya elimu, tuwe na kilimo cha kisasa na kuanzisha viwanda kwa ajili ya vijana wetu nchini,” alisema.
SUMAYE
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye alipanda jukwaani saa 9:55 alasiri na kuonya kuwa kama CCM haitakubali kushindwa inaweza kusababisha machafuko.
“Nchi hii iko kwenye mfumo wa vyama vingi na ili viwe na maana lazima kila chama kiwe tayari kushindwa kama hakijafanya vizuri, lakini CCM hakitaki, hali hii ni hatari sana.
“Libya, Misri na Tunisia zimefika zilipofikia kwa sababu waliokuwa kwenye madaraka walikuwa hawataki kuachia na kukandamiza watu. CCM isipokubali mabadiliko itakuwa inataka yale ya Gadafi,” alisema Sumaye.
Alifananisha matusi yanayotolewa na wapinzani wao dhidi yake na Lowassa kuwa ni sawa na kumpiga teke chura.
“Wanatengeneza timu za kututukana, lakini nawaambia hapo ni sawa na kumpiga teke chura. Lowassa alitoka serikalini miaka minane iliyopita na tume ya Bunge ilisema hakukuwa na jambo lililomgusa moja kwa moja...alijitosa ili kumuokoa rais na Serikali yake,” alisema.
Waziri Mkuu huyo pia aliibeza hoja ya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kuwa hataweza kupambana na rushwa kwa sababu tayari ameonyesha udhahifu katika wadhifa aliokuwa nao wa Waziri wa Ujenzi.
“Utabadilishaje Tanzania wakati leo hii wewe ni waziri, lakini kwenye mizani kumejaa rushwa?
“Ataitoa wapi nguvu ya kupambana na rushwa, ndani ya CCM huwezi kufanya kitu chochote,” alisema.
Sumaye pia alisema kitendo cha kutoweka jina la chama katika mabango ya mgombea urais wa CCM kinaonyesha kuwa ndani ya chama hicho hali ni mbaya.
“Mabango yanasema “Chagua Magufuli” hayasemi “Chagua CCM”, kama anajua CCM haimpeleki kokote si angekuja Ukawa?
“Mimi niko Ukawa, lakini sigombei urais, kazi yangu ni kuwakomboa wananchi,” alisema Sumaye na kuongeza kuwa “CCM ni shida”.
MBOWE
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitamba kuwa wananchi wote wako tayari kufanya mabadiliko.
“Tumekwenda Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora na leo (jana) tuko Dar es Salaam, nchi imeshalegea na iko tayari kwa sababu ya Lowassa,” alisema Mbowe.
Huku akiwaelekeza wananchi kuzungusha mikono kama ishara ya kufanya mabadiliko, Mbowe alionya kuwa kama machafuko, basi yataletwa na NEC kutokana na kitendo chao cha kujaribu kuibeba CCM.
“Sasa hivi CCM haibebeki hata ukileta mbeleko, wanawatumia baadhi ya watu kumchafua Lowassa, Sumaye na wote walioondoka CCM...wapuuzeni watu wamefika bei,” alisema.
MDEE
Mgombea ubunge katika Jimbo la Kawe, Halima Mdee, aliomba idhini ya viongozi wa chama hicho kufanya maandamano ya kuishinikiza NEC kuacha kufanya hujuma.
“Tuna mashaka na zoezi linaloendelea la uhakiki, kuna watu wanaandikisha vitambulisho vya vijana na kina mama, CCM na NEC wanataka kufanya uhuni.
“Tunaomba kauli yenu kama ikibidi tuandamane hadi NEC tukakinukishe, tutafanya hivyo,” alisema Mdee.
Kwa mujibu wa Mdee,katika jimbo hilo wamefanikiwa kutatua migogoro ya ardhi katika eneo la Chasimba na Nakerekwa, lakini bado kuna mgogoro katika eneo la Boko kwa Sonji ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 20 na katika eneo la Magereji lenye vijana zaidi ya 4,000.
“Mtaji wa vijana hawa wa gereji ni zaidi ya Sh bilioni tano na wamekaa hapa tangu mwaka 2007, lakini leo hii wanaambiwa waondoke,” alisema.
MWALIMU
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu, alisema CCM wameishiwa sera na sasa wanafanya matamasha ya burudani.
“Magufuli anazunguka nchi nzima kufanya matamasha ya burudani badala ya kunadi ilani ya chama chake...ukiingia muachie wizara ya utamaduni,” alisema Mwalimu.
KUWASILI UWANJANI
Maelfu ya wananchi walianza kuwasili viwanjani hapo saa 3 asubuhi na ilipofika saa 7 mchana uwanja ulikuwa umejaa.
Baadhi ya watu walilazimika kupanda juu ya miti na wengine kupanda juu ya mapaa ya Shule ya Msingi Bunju A ili waweze kushuhudia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huo.
Waendesha bodaboda walikuwa ni kivutio pekee katika mkutano huo kwani wengine walionekana kuendesha pikipiki kwa mbwembwe kubwa huku wakipaa juu na wengine walikuwa wakizunguka uwanja huo mara kwa mara.
Baadhi ya watu walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kama vile ‘Dk. Slaa kiapo cha kanisa kimekuponza uchizi unakunyemelea’ na ‘ulipo tupo’.
JIMBO LA KIBAMBA
Katika mkutano uliofanyika Jimbo la Kibamba kwenye Uwanja wa Mbezi Mwisho, Lowassa alisema hana muda wa kubishana na wanachama wa CCM wanaomtukana majukwaani, na kwamba watakutana katika sanduku la kura.
“Mahaba yananifanya nijiamini, ndiyo maana ndugu zangu wanahangaika nikiwa na nguvu ya umma kama hii, nawaambia tukutane kwenye sanduku la kura,” alisema.
Lowassa alisema endapo watu wanataka mabadiliko katika maeneo mbalimbali ikiwamo elimu, wanapaswa kuandaa shahada zao na kuwapigia kura wagombea wa Ukawa Oktoba 25.
Naye Sumaye alisema katika uchaguzi wa mwaka huu CCM lazima itoke madarakani hata kama haitaki.
“CCM hakitaki kutoka madarakani hata kama watu hawakitaki, wanatumia hila zote, tunasema safari hii mtatoka tu ,mnahangaika kuchafua viongozi, mnanihangaika hadi mimi ambaye sigombei,” alisema Sumaye.
Alisema kitendo cha wanachama wa CCM kujipanga na kumtukana hakisaidii badala yake kinamwongezea nguvu ya kupigania maendeleo.
Sumaye alisema alikihama chama hicho kwakuwa kimeshapoteza matumaini ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
MNYIKA
Mgombea ubunge Jimbo la Kibamba, John Mnyika, alimfanisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na Samson wa kwenye Biblia aliyedanganywa na Delila.
“Mnamfahamu Samsoni wetu? Alisema tumemchukua mtu chooni tukamwingiza chumbani, amesahau kwamba yeye katoka chumbani ameenda chooni, msiendelee kumsikiliza Samsoni, mpuuzeni hana jipya.
“Mzee wetu kadanganywa ameenda chooni kuwaunga mkono CCM,” alisema Mnyika.
Katika hatua nyingine, alimtaka Lowassa akiingia madarakani kuangalia tatizo la maji ambalo ndilo kubwa ndani ya jimbo la Kibamba.
Naye Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, aliituhumu CCM kuwa inatumia Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) kukwepa kodi ya mafuta ili ikusanye Sh bilioni 50 za kununua shahada za kupigia kura.
“Kuna mkakati wa kuitumia TRA kuingiza mafuta ambayo hayatalipiwa kodi ili wapate Sh bilioni 50 kwa ajili ya kuwasaidia kununua shahada za kupiga kura. Tunawaambia tumewabaini na waache mara moja huo mchezo, tunataka watukabidhi nchi ikiwa na hazina ili tuweze kuleta mabadiliko ya kweli,” alisema Mbowe.
Alisema anao ushahidi ju ya hilo na kuongeza kuwa CCM inaweweseka mwaka huu.

Mkutano Ukawa wakatishwa kwa vurugu

Katibu wa Chadema mkoa wa Mtwara, Willy Mkapa

JESHI la polisi mkoani Mtwara jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi ili kurejesha hali ya amani katika mkutano wa Chadema uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa mjini hapa.
Mkutano huo ambao vyama vya siasa vya upinzani vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) vilialikwa, ulikuwa na lengo la kuwatambulisha wasanii wa filamu na wa muziki wa kizazi kipya wanaomuunga mkono mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa.
Akizungumzia tukio hilo jana, Katibu wa Chadema mkoani hapa, Willy Mkapa, alisema lengo la tamasha hilo lilikuwa kumnadi mgombea wa urais pamoja na mgombea wa ubunge kupitia Ukawa, na kuwatambulisha wasanii wanaomuunga mkono Lowassa.
Alisema baada ya wasanii hao kutumbuiza na kuwadia muda wa hotuba ndipo vurugu zilipoanza ambapo inadaiwa kulikuwa na kikundi cha wafuasi wa mgombea ubunge wa Mtwara Mjini kupitia NCCR –Mageuzi, Uledi Hassan, kutaka mkutano huo usimnadi mgombea ubunge badala yake umnadi mgombea urais pekee.
Wafuasi hao wanadai kuwa wao kama NCCR wanamgombea wao, Chadema wana mgombea wao na vivyo hivyo CUF wana mgombea wao, hivyo isingekuwa vyema kumnadi mgombea mmoja.

Na baada ya mabishano yaliyochukua dakika kadhaa ndipo jeshi la polisi lilipoingilia kati na kutaka kuwaondoa wafuasi hao mkutanoni hapo.
Hali hiyo ilizua taharuki na polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi na kufyatua risasi hewani na kisha kufanikiwa kumkamata kijana mmoja aliyedaiwa kuongoza wenzake na kuondoka naye hadi Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa.
Katibu huyo wa Chadema alisema kwa mujibu wa viongozi wa juu wa vyama vinavyounda Ukawa, Jimbo la Mtwara Mjini anayetakiwa kuwa mgombea ni Nachuma Maftaha wa CUF na kwamba Chadema wanamuunga mkono, ndiyo maana mgombea wao amejitoa, lakini NCCR- Magenzi bado wanalazimisha mgombea wao awanie ubunge jimboni humo.

NUH MZIWANDA: SIONI TATIZO KWA MSANII KUONESHA MAHABA KWA CHAMA ANACHOKIPENDA


Nuh Mziwanda amewataka wasanii kuwa wazalendo kwa kuonyesha hisia zao za vyama vya siasa na kuonyesha ushirikiano katika kuhamasisha.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio leo, Nuh alisema maendeleo yatakayopatikana ni manufaa kwa watanzania wote kwa ujumla.

“Wewe ukiwa msanii sio kwamba sio mwananchi wa kawaida,” alisema.

“Wewe pia unahitaji kutawaliwa vizuri. Unahitaji utawala mzuri ambao utaongoza hata kazi zako ziende vizuri.
 Kwahiyo ni vyema mtu ukajua upo upande gani, huo ni upendo wa nchi yako na ni mzalendo. Kila binadamu anapenda uongozi mzuri ndio maana kila mtu akiwa na akili timamu ana haki ya kuchagua chama anachokitaka,” aliongeza.

“Lakini sisi wasanii tusijisahau tukawa tunashindwa kuweka hisia zetu kwaajili ya maslaHi ya nchi yetu. Unaogopa kuweka wazi wewe ni chama gani, unampenda mwanasiasa gani! Sisi ni vioo vya jamii tunaangaliwa pia na watu na kuna watu wahitaji ushauri au ufafanuzi juu ya viongozi waliotangaza nia. Kwa sisi inatubidi tuwe mfano kwanza kabla ya wananchi.”

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA WAGANGA WAKUU LEO JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza na wananchi kwenye ufunguzi wa  mkutano wa Mwaka wa waganga wakuu wa Mikoa,halmashauri na wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa hapa nchini  katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo kwa wataalamu waoshiriki jitihada za kudhibiti Ugonjwa wa Ebola Afrika Mashariki, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Dnan Mmbando jijini Dar es Salaam leo.




 
 Sehem ya wananchi waliohudhulia katika mkutano huo.
 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib  Bilal akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mabalimbali leo jijini Dar es Salaam .
(Picha na Emmanuel Massaka)
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

CHAT BOX

Post zilizo tumwa

Recent Posts Widget

Tangaza Biashara yako mtandaoni

TANGAZA BIASHARA NAMI HAPA KWA BEI NAFUU KABISA

Unaweza kutangaza biashara yako sasa na hlmservice pia uta pata kujua mambo mengi ambayo mbali na biashara yako unaweza ukatengeneza pesa kwa namna moja ama nyingine kama jinsi nilivo elezea katika Makala za nyuma hapo

Wafanya biashara wengi wanatumia mda mwingi namna gani ya kukuza biashara zao ,Ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unahitaji kuitangaza biashara yako ili kuwa na mtandao mkubwa na wateja wako ,ni vyema ukatangaza biashara yako katika mitandao ili bidhaa zako zijulikane kwa haraka na upesi .

Pia wewe mfanya biashara ukiitaji kuwa na blog yako wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini , bei ni nafuu kabisa

Pia ukiitaji kuitangaza biashara yako kupitia blog yangu bei ni ndogo kabisa huu ni wakati wako wewe mfanya biashara

+255758061575 & +255684860817

henrylameck@gmail.com

henrylameck90@yahoo.com

Tukuyu Tour & Safari

Vadacom Ni Zaidi

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Kilimo Kwanza

Hlm servise

Latest movie

Movies

Computer books

Computer books