Mkazi wa
Sinza Bi. Clara Joseph (kulia) akiifurahia zawadi yake ya fulana na
mfuko alivyokabidhiwakwenye shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani
lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya sanaa vilivyopo
Legho, Sinza jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Meneja mipango na
Matukio-SBL Lulu Mduma na (kulia) ni Mtangazaji wa redio Efm na
mshereheshaji wa Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash.
Mkazi wa
Sinza, Prosper Minja akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Meneja
Mipango na Matukio-SBL Lulu Mduma katika shindano la Tusker Fanyakweli
Kiwanjani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya sanaa
vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam ambapo baa 7 zilizopo kwenye
mkondo mmoja ziliibuka baa za wiki kwenye promosheni hiyo ya Tusker
Fanyakweli Kiwanjani baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina
Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.
Mkazi wa
Mwanza na mpenzi wa bia ya Tusker Hillary Minja (katikati) ambaye
alikuwepo kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani akimuelezea
Mtangazaji wa redio Efm na Mshereheshaji wa promosheni hiyo ya Tusker
Gadner Habash (kushoto) kwanini ameichagua bia hiyo kwenye hafla ya
kuzipongeza baa 7 zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa pamoja ziliibuka
baa za wiki kwenye shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani
lililofanyika katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar
es salaam. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa
junction, Chua pub na Lucy pub Anaeshuhudia (kulia) ni balozi wa bia
hiyo Veronica Mbilinyi.(VICTOR)
Mpenzi
wa kinywaji cha Tusker na mkazi wa Sinza Rosemary John (Kulia) akifurahi kwa
pamoja na Meneja Mipango na matukio-SBL Lulu Mduma (kushoto) baada ya
kukabidhiwa zawadi ya fulana kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani
ambayo ilifunga kambi katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini
Dar es salaam kusherekea ushindi wa baa zaidi ya sita zilizo kwenye mkondo
mmoja ambazo kwa pamoja ziliibuka washindi wa wiki wa promosheni hiyo
inayoendeshwa na bia ya Tusker. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina
Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.
Mkazi
wa Kimara Kona, Thomas Kimaro (katikati) akipokea zawadi yake ya fulana toka
kwa Meneja Mipango na Matukio-SBL Lulu Mduma (Kushoto) katika shindano la
Tusker Fanyakweli Kiwanjani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya
sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam (Kulia) ni Mtangazaji wa
redio Efm na mshereheshaji wa Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner
Habash.
Kampeni
ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kwa
udhamini wa bia bora Afrika ya Tusker wiki hii imekuja na mvuto wa aina yake
baada ya kuzikutanisha na kuzifanyia sherehe baa mbalimbali zilizopo kwenye
mkondo/mtaa mmoja.
Tukio
hilo ambalo lilionekana kuwafurahisha wapenzi wa bia ya Tusker lilifanyika
wikiendi ya Jumamosi katika mtaa wa Legho, Sinza jijini Dar es salaam ambapo
baa zaidi ya 6 zote kutoka Sinza ziliungana kushiriki katika sherehe hizo. Baa
hizo ni:- Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na
Lucy pub.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa sherehe hizo, Meneja Masoko wa bia ya Tusker Bi. Nandi
Mwiyombella alisema mpaka kufikia sasa kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani
imepokelewa vyema na wateja wa bia hiyo jijini Dar na hata mikoani ambapo
kampeni hiyo pia inaendelea.
“Promosheni
hii ni muendelezo wa Kampeni ya Tusker Fanya Kweli kama inavyoonekana kwenye
mabango na matangazo ya radio pia ni kampeni inayolenga kuleta muamko wa hamasa
kwa watanzania waweze kutekeleza malengo yao waliyoyapanga“.
Alisema
kuwa katika maisha baadhi ya malengo yanayotarajiwa ni pamoja na kujenga
nyumba, kufunga ndoa, kununua gari kuanzisha biashara na kadhalika. Mafanikio
ni hatua na kila hatua inastahili pongezi na kusherehekea matunda ya mafanikio
hayo,bia ya Tusker inatambua juhudi za watanzania ambapo juhudi lazima ziendane
na utekelezaji na katika kufanya hivyo basi mtanzania anapiga hatua hivyo
kupitia Kampeni hii Bia ya Tusker inampongeza mtanzania kwa kila hatua
anayopiga.
Tunaamini
kwamba kupitia Kampeni hii ujumbe huu utawafikia watanzania wote kwa urahisi
zaidi.Bia ya Tusker inatoa hamasa na kusema tufanye kweli na Tusker inatambua
kila hatua ya maendeleo iliyopigwa.
Bi.
Mwiyombella aliongeza kuwa sherehe za Tusker Fanya Kweli Kiwanjani pia
zinalenga kujenga uaminifu kwa wateja na kurudisha shukrani kwao huku
wakisherekea kwa pamoja na bia waipendayo ya Tusker. Sherehe hizi za mkondo wa
baa tofauti ni muendelezo wa kampeni ya Fanya Kweli Kiwanjani; ikiwa na
mkusanyiko wenye ari na muamko zaidi na hivyo ni burudani zaidi sambamba na
zawadi nyingi zaidi kwa wateja.
Kampeni
ya Fanya Kweli Kiwanjani itaendelea mpaka mwisho wa mwezi wa kumi huku sherehe
za mkondo wa baa zikitegemewa kuwafikia pia mashabiki wa bia ya Tuskerwaliopo
Arusha na Mwanza kabla ya kampeni kufikia tamati.
0 comments:
Post a Comment