“Tumeamua kuufahamisha umma juu ya jambo hili kutokana na taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitafanya mkutano wa uzinduzi wa kampeni keshokutwa katika uwanja huo,” alisema Mwambene.
Alisema walipata barua ya maombi kutoka Chadema Agosti 12 wakiomba uwanja huo kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni zao na kwamba walishawapatia majibu kwamba hakuna chama cha siasa kitakachoruhusiwa kutumia uwanja huo kutokana na mihemuko na hamasa za kisiasa inayoweza kujitokeza miongoni wafausi wa vyama na kusababisha uharibifu.
Alisema walichukua uamuzi huo kwa busara ili kuufanya uwanja wa Taifa ubaki kwa ajili ya shughuli za michezo tu.
Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, alisema hawajapata taarifa zozote kutoka serikalini zaidi ya kusikia kupitia vyombo vya habari.
Makene aliongeza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kuficha aibu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuhofia wingi wa watu
“Serikali inapaswa kutambua kuwa uchaguzi unaamua hatima ya nchi husika kwa kuzingatia demokrasia, hivyo wanachokifanya ni kuvinyima vyama vya upinzani haki ya msingi kwa ajili ya shughuli mhimu kwa kigezo cha kuvunja amani kitu ambacho si sahihi,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Makene, hawatapoteza muda kubishana na Serikali bali watatafuta eneo lingine la kufanyia mkutano huo na watatoa taarifa kwa wananchi na wafuasi wote wa Ukawa nchini.
0 comments:
Post a Comment