WAGOMBEA urais wanaotarajiwa kuwa
na mchuano mkali kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu, Dk. John Magufuli
(CCM) na Edward Lowassa (Chadema), wanarejesha fomu za kugombea nafasi hiyo leo
kwenye Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Tofauti ni ilivyokuwa takriban
wiki mbili zilizopita wakati wanasiasa hao walipokwenda kuchukua fomu hizo
tayari kwa kutafuta wadhamini sehemu mbalimbali nchini, leo watalazimika kwenda
kimyakimya.
Wakati wa kuchukua fomu ambapo Dk.
Magufuli ndiye aliyekuwa wa kwanza, shughuli katikati ya Jiji la Dar es Salaam
zilisimama kwa muda kuwapisha wanachama wa CCM waliomsindikiza na kisha
kuhitimisha kwa hotuba kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Mtaa wa
Lumumba.
Siku mbili baadaye, Lowassa naye
alifunga mitaa kadhaa ya jiji kwa maandamano yaliyoanzia Buguruni hadi katikati
ya jiji, kisha kuelekea Makao Makuu ya Chadema Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, huku
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akishindwa kuhimili mikiki mikiki hiyo na
kwenda ‘kupumzishwa’ Muhimbili.
Kwa kuheshimu shughuli za wakazi
wengine wa Dar es Salaam wasiojihusisha na siasa za moja kwa moja, Jeshi la
Polisi lilizuia maandamano ya aina hiyo na kuagiza kuwa wagombea hao sasa
watasindikizwa na watu saba tu kwenda NEC kurejesha fomu.
Kwa hiyo leo, Dk. Magufuli (55)
ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya
ufisadi ya Richmond, Lowassa (62), pamoja na wagombea wa vyama vingine,
watarejesha fomu hizo bila mbwembwe zozote.
“Magufuli atawasilisha fomu zake
saa tano asubuhi ya kesho (leo) akifuatana na mgombea mwenza, Samia Suluhu
Hassan,” inasomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa jana na CCM.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa
ama na Chadema au Ukawakuhusu muda atakaorejeshafomu Lowassa ingawa naye
atafanya hivyo leo kwa kuwa ndio siku ya mwishoiliyopangwa na NEC.
Baada ya Dar Magufuli kuanzia
Katavi
Mara baada ya kurejesha fomu,
Magufuli atapata fursa ya kuzungumza na Watanzania wakati wa uzinduzi rasmi wa
kampeni za chama hicho uliopangwa kufanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini
Dar es Salaam kesho kutwa.
Ingawa bado ratiba rasmi
haijatolewa, Raia Tanzania linafahamu kwamba Jumatatu ijayo, Dk. Magufuli
ataanza kampeni za mikoani katika Mkoa wa Katavi kisha Rukwa na baadaye Mbeya.
Kwa upande wa Ukawa, hadi jana
jioni hakukuwa na taarifa zozote kuhusu wapi watafanyia uzinduzi wa kampeni na
baada ya hapo watakwenda mkoa gani.
Juzi, ombi la Ukawa kuzinduliz
kampeni Uwanja wa Taifa, lilikataliwa na serikali.
Wakati huo huo, NEC imewataka
viongozi wa dini nchini kuacha kuonyesha hisia zao juu ya chama au mgombea
wanayemtaka na kuepuka kushawishi waumini wao kuegemea upande wowote ili
kufanikisha kufanyika uchaguzi wa huru na haki.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, wakati tume hiyo ilipokutana
na viongozi wa dini kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.
Aliwaomba viongozi hao kutumia
mimbari kuwaelimisha na kuwafahamisha wapiga kura waweze kufanya uamuzi baada
ya kupata taarifa sahihi na kumchagua kiongozi anayemtaka.
“Ikumbukwe kwamba sheria ya
uchaguzi zinakataza viongozi wa dini kutumika katikia masuala ya kisiasa kama
vile kufanya kampeni za uchaguzi katika maeneo yenu ya ibada. Kamwe msiruhusu
maeneo yenu yatumiwe na vyama vya siasa kama majukwaa ya kisiasa,” alisema Jaji
Lubuva.
0 comments:
Post a Comment