Wewe mtanzania unahitaji kujua computer ni kitu
gani kabla ya kuanza kuifanyia kazi pia unabidi kufahamu umuhimu wa kuwa na
computer nyumbani kwako ,Leo nitakuwa sijakutendea haki kama sita kufahamisha
maana ya computer pamoja na matumizi ya computer ,Kuna maana nyingi sana ya
kifaa computer ,utaweza kuelezea maana za computer kutokana na matumizi ya kila
siku lakini kwa maana kuu tuta sema kwamba “Computer ni Kifaa kinacho tumia
umeme kinacho weza kufanya mambo makuu matatu ambayo ni kuhifadhi data mbali
mbali ambazo unaweka ndani ya computer ,Baada ya kuweka data zako katika
computer basi zita kuwa processed ndani ya computer na mwisho wa yote tuta pata
output ambazo ni matokoe ya data kuwa processed”
Vile vile Computer tutaweza
kusema ni kifaa kinacho weza kukurahisishia wewe mtanzania kuingia internet na
kufanya shughuli zako mtandaoni mfano mzuri unapo tuma email, unapo chati
katika mitandao ya kijamii kama facebook,twiter,nk tutajifunza mengi kuhusu
internet endelea kusoma mada hii ili kujua mengi Zaidi ,
Mambo
ya msingi kuhusu intaneti
Wavuti
ni nini, na ni jinsi gani unavyoweza kuifanyia kazi?
Unavyochunguza
vidokezo juu ya usalama katika Vizuri Kufahamu, unaweza ukawa na maswali kadhaa
kuhusu wavuti ni nini na jinsi ya kutumia aina maarufu ya huduma mtandaoni.
Tafadhali angalia majibu haya kutoka Googlers na pata maelezo zaidi kuhusu
kuingia mtandaoni, kupata maelezo na kuabiri katika mtandao, na kuunganisha na
kushiriki mtandaoni.
Kuingia mtandaoni
Intaneti ni nini?
Intaneti
ni mtandao wa kompyuta zilizoenea duniani kote zote zikiwa zimeunganishwa moja
kwa nyingine. Unapojiunga kwenye Intaneti unakuwa na ufikiaji wa World Wide
Web, ambayo ni sawa na maktaba iliyojaa kurasa za maelezo.
Unaunganishwa vipi kwenye Intaneti? Shughuli
ya ISP ni ipi?
Kabla hujaanza kuuchunguza
mtandao, utahitaji kuweka mpango na ISP. ISP, au Mtoa Huduma za Intaneti, ni
kampuni inayokuruhusu kufikia Intaneti na huduma nyingine za mtandao. Wanatoa
njia tofauti za kuunganishwa ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kebo, fiber optics
au Wi-Fi. Muunganisho hizi tofauti huamua kasi ya ufikiaji wako wa mtandao.
Baada ya kuona maana ya computer
na internet basi tuangalie umuhimu wa kuwa na computer ni upi na tutatumia vipi
computer kuinua hali zetu za kiuchumi
Computer ina matumizi mengi sana
ukiwa nyumbani,kwako mwanafunzi, pia hata maofisini ,pia unaweza ukajiajili
kupitia computer yako hapo ulipo
Kwa mwanafunzi utaweza kusomea
computer pamoja na kutafuta mengi kwenye internet, kwa mfanya biashara utatunza
kumbukumbu zako za kibiasha pia hata za kiofisi
Unaweza kutengeneza pesa kupitia
computer yako ya nyumbani kama utakuwa mbunifu wa kujitangaza kupitia computer
yako.Blogger ni njia pekee inayo weza kuitangaza biashara yako kwa kasi na kwa
watu wengi duniani ,Blog ni mfano wa website ambayo unaweza kuweka matangazo
yako ya kibiashara pamoja na kujitangaza wewe ni nani ?
Ni rahisi sana kutengeneza blog
yako na kujitangaza Zaidi, pia nitakuelekeza jinsi ya kuanzisha blog yako ya
kibiashara pamoja na kupata muonekano mzuri zidi wa blog yako
Mara nyingi unapo tengeneza blog
itakulazimu uwe katika internet lakini kuna njia mbali mbali za kutengeneza
blog kuonekana katika muonekano mzuri Zaidi kwa kutumia Microsoft word,
Microsoft publisher pamoja na Excell, Sio hivo kuna lugha mbali mbali za
kutengeneza kurasa za blog yako
Kuna mfano wa lugha ina itwa HTML, CSS, JavaScript ni
lugha nzuri za kutengeza kurasa zako za blog yako yote hayo utayapata hapa
katika tovuti yetu hii ya hlmservice.
COMPUTER GANI INA
FAA KWA MATUMIZI YAKO
Chagua
computer inayo weza kukidhi mahitaji yako ukizingatia uwezo wa computer je
unahitaji utumie katika matumizi gani, Kwa mfano wewe ni designer na katika
designing yako unatumia program kubwa kama adobe photoshop basi chagua computer
yenye ukubwa mkubwa kwa kuangalia Hard
Disk Isiyo pungua 500Gb na processor 2.20GHz na RAM(Random Access Memory) Sio chini ya 2.0Gb ,
kwa matumizi ya kawaida kabisa pia fuata vigezo hapo juu lakini itapendeza kama
utachukua computer yenye ukubwa wa wastani ili kuifadhi kumbukumbu zako rahisi
na kwa wingi Zaidi
Unaweza
ukawa na home network nzuri inayo weza kukidhi mahitaji yako kabisa kwa kutumia
simu yako ya smart phone, Hapa inakuwa haina haja ya kutumia modem kutengeneza
network nyumbani hata oficine ,Kupitia simu yako ya smartphone unaweza
kutengeneza wireless inayo weza kumudu kwa computer Zaidi ya tatu hadi nne
kikubwa ni kujiunga vifurushi vya internet kama kawaida ya vifurushi vya
mitandao yote alafu tengeneza wireless yako ufurahie internet na yenye kasi
Zaidi
Jinsi ya kutengeneza wireless kwa kutumia smartphone yako fuata
hatua zifuatazo
Hatua
ya kwanza
Ingia Katika sehemu ya setting
kwenye simu bofya Mahali pameandikwa More..Utaona
maelezo haya juu kabisa pameandikwa Wireless&Networks chini yake
utaona
Airplane Mode
Vpn Settings
Tethering & Portable hotspot
Mobile Networks
Hatua
ya pili
Bofya mahali wameandika Tathering &
Portable hotspot itakuonesha jinsi ya kuiwasha wireless yako lakini
kabla ya yote unahitaji kuitengeneza kwa jina unalo taka kwa kubofya mahali
pameandikwa Set-up Wi-Fi hotspot ,Andika jina upendalo pia kuna mahali pa
kuweka passwork kama unahitaji kwa jili ya kuzuia watu wengi kutumia wireless
yako basi andika passwork na iwe siri kwako tu ,Endapo utasambaza password yako
utaona matumizi yako ya bundle ni makubwa kwa sababu utakuwa umeruhusu watu
wengi watumie wireless yako
Hizo hatua mbili juu ni kwa wale
watu wanao tumia simu za Android lakini kwa wanao tumia windows phone ni rahisi
Zaidi kwani utaenda mahali pameandikwa setting halafu Internet sharing,Uta seti
password na jina la wireless yako.
Kabla ya kufanya yote hayo
hakikisha computer yako ina support wireless kama hapana basi angali kama kuna
driver za wireless kama computer itakuwa hai support basi zoezi hili litakuwa gumu
kwako.
Asante sana mpenzi msomaji wa
Makala yangu hii ya leo mungu akubariki usikose kusoma habari nyingi Zaidi na
Zaidi mada zinazo kuja mbele ni nzuri Zaidi tutafundisha jinsi ya kuinstall
windows katika computer yako ,jinsi ya kuiandaa flash yako iweze kuboot window
moja kwa moja badala ya kutumia CD” Mimi mwandishi wako henry
Lameck unaweza wasiliana nami moja
kwa moja katika email yangu hapa chini
pia +255765327325
+255766518985
Technologia Ya Computer ~ Computer Services >>>>> Download Now
ReplyDelete>>>>> Download Full
Technologia Ya Computer ~ Computer Services >>>>> Download LINK
>>>>> Download Now
Technologia Ya Computer ~ Computer Services >>>>> Download Full
>>>>> Download LINK HC