umojannguvu.blogspot.com

Saturday 22 August 2015

Mgombea ubunge wa Chama cha Wananchi (CUF) amedai kutekwa kutishwa na kuporwa fomu za kugombea katika jimbo la Shaurimoyo





Mgombea ubunge wa Chama cha Wananchi (CUF) amedai kutekwa, kutishwa na kuporwa fomu za kugombea katika jimbo la Shaurimoyo, Unguja.

Mgombea huyo, Abdi Seif Hamad, alidai kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 17, mwaka huu majira ya asubuhi katika maeneo ya jimbo hilo. Alidai kuwa akiwa maeneo hayo wakati akitafuta wadhamini, ghafla kikatokea kikundi cha watu wapatao wanane wakiwa wamejifunika nyuso na kumteka, kumtisha kisha kumnyang’anya fomu ambazo alikuwa ametoka kuzichukua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

“Namshukuru Mungu hawakunijeruhi wala kunipiga, waliniambia wanachokihitaji ni fomu ambazo nilizokuwa nimebeba mfukoni,” alidai Abdi. Alidai kuwa baada ya kumnyang’anya fomu hizo walimuachia na kwenda kuripoti kituo cha polisi cha Ng’ambu na kupewa namba RB/6085/2015 kisha kuripoti Nec na jana alipewa fomu nyingine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema hajapata taarifa za kuripotiwa kwa tukio hilo. “Watu wangu waliopo katika doria siku ya mkutano wa Chadema uliongozwa na mgombea wa urais kupitia chama hicho, Edward Lowassa, ndio walipata taarifa hiyo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alitoa taarifa ya tukio hilo akiwa juu ya jukwaa akiwahutubia wananchi,” alisema Mkadam. CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

CHAT BOX

Post zilizo tumwa

Recent Posts Widget

Tangaza Biashara yako mtandaoni

TANGAZA BIASHARA NAMI HAPA KWA BEI NAFUU KABISA

Unaweza kutangaza biashara yako sasa na hlmservice pia uta pata kujua mambo mengi ambayo mbali na biashara yako unaweza ukatengeneza pesa kwa namna moja ama nyingine kama jinsi nilivo elezea katika Makala za nyuma hapo

Wafanya biashara wengi wanatumia mda mwingi namna gani ya kukuza biashara zao ,Ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unahitaji kuitangaza biashara yako ili kuwa na mtandao mkubwa na wateja wako ,ni vyema ukatangaza biashara yako katika mitandao ili bidhaa zako zijulikane kwa haraka na upesi .

Pia wewe mfanya biashara ukiitaji kuwa na blog yako wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini , bei ni nafuu kabisa

Pia ukiitaji kuitangaza biashara yako kupitia blog yangu bei ni ndogo kabisa huu ni wakati wako wewe mfanya biashara

+255758061575 & +255684860817

henrylameck@gmail.com

henrylameck90@yahoo.com

Tukuyu Tour & Safari

Vadacom Ni Zaidi

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Kilimo Kwanza

Hlm servise

Latest movie

Movies

Computer books

Computer books