MAMBO MUHIMU YA
KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA LAPTOP.
Kwa Mwanafunzi, Mfanyabiashara, Photographer au
videographer. Mcheza Games, Mtumiaji wa Nyumbani /matumizi ya kawaida.
1. Wanafunzi
Mambo makuu kwa mwanafuzi ni bei ya kubebeka kwa laptop yenyewe. Laptop
inayoweza kubebeka kutoka darasa mpaka darasa, au darasani mpaka kwa sam muuza
chipsi, ndio cha msingi , kwa hiyo kwa wanafunzi wengi huwa ni Netbooks ambazo
hazina gharama kubwa, ni ndogo, inatumia nishati ndogo na ni around tshs
450,000-700,000. Ubaya wake ni kwamba hizi huwa na screen ndogo na hutumia
single-core CPUs ambazo zimepunguzwa nguvu.
Option nyingine ni laptop yenye inchi 13,
nyembamba, ambayo portability yake (uwezo wa kubebeka) ni mzuri, na inapendeza
zaidi wa kuandikia au kutumia ukiwa umekaa sehemu tulivu na sio haraka haraka.
CPU zake ni dual-core na mara nyingi huja na optical drives. Mfano mzuri ni
MacBook za Apple zenye inchi 13.
Nini Cha Kuzingatia: At least 1GB ya RAM; 160GB au
zaidi za HDD; inchi 13 au chini ya hapo.
2. Mfanyabiashara
Wale ambao mara nyingi huwa barabarani huitaji mashine iliyo faster, inaydumu
na charge na zaidi ya yote
ThinkPad za Levono na Latitude za Dell ni mifano
miwili mizuri ya laptop zilizotengenezwa zikimlenga mfanyabiashara (au kwa
lugha rahisi, anayesafiri mara kwa mara) . Bidhaa zote mbili zina security
nzuri na imara, pia hardware za in-built software zake zinafanya kazi vizuri na
OS (Operating System) yoyote e.g windows, Ubuntu, etc (lakini sio Mac, ).Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 160GB au zaidi
kwa Hard Disk; 12 mpaka 15-inch display; Windows Vista Professional au Windows
7 Professional; mobile broadband modem.
3. Mpigapicha na/au Videographer
Wachezaji wa games sio watu pekee wanaohitaji processor yenye nguvu, graphics
za ukweli na hard disk space kuuuubwa. Kwa wale ambao wanatengeneza
high-definition video or high-resolution photographs huitaji mashine inayojitosheleza
hasa! Nimekuwa mpenzi mkubwa sana wa video producing. Miaka ya nyuma nikaanza
kujifunza After Effects, FinalCut, etc. Ila kilichosumbua ilikuwa ni mashine.
PC yangu RAM 1GB, hard disk 80 GB na vikolombwezo vingine vya kimaskini.
Nikaishia kwenye Windows Movie Maker
MacBook Pro inch 15 mpaka 17 zile za Apple ndio
maarufu na nzuri kwa kazi hii (expensive though). MacBook ni nzuri pia kwa
sababu software ya Final Cut, ambayo ndio maarufu DUNIANI kote kwa video
producing, inapatikana kwenye Mac pekee. (Adobe’s Photoshop inapatikana kwenye
platform tofauti tofauti, hivyo usijali).
Cha msingi hakikisha SANA SANA SANA kuwa una RAM
kubwa…….. 8GB za RAM ndio penyewe. Pia hard disk ya 500GB ingependeza sana, kwa
sababu redering in real-time inahitaji RAM/processor faster na inakula space
hasa.
Cha kuzingatia: 4GB-8GB of RAM; Hard Disk ya 320GB
yenye uwezo wa 7,200rpm, yaani 7,2000r per minute (usijali kama huelewi
inamaanisha nini, wewe mwambie muuzaji hivyo ukiwa na uso mkavu..bhaaaas);
17-inch or larger display.
4. Wachezaji Games
Games za sasa hivi zinafika mpaka 20GB na hiyo setup tu! Mambo yanaanza kuwa
mengi kama video card, sound drivers, na makolombwezo kibao! Kama wewe ni
gamer, basi utahitaji desktop computers, zenye flexible upgradeability, faster
components, na yenye uwezo wa kupoa haraka.Ila kwa siku za hivi karibuni,
laptops zinazowafaa gamers zina-hit sana.
Ningependekeza kuanzia Core 2 Quad za Intel na Core
i7 CPUs kwa 3D gaming, kwa sababu zina GPU nzuri ,kama GeForce N260 za Nvidia.
Ya kuzingatia: 4GB mpaka 8GB za RAM; 320GB au zaidi
kwa Hard Disk; display ya inchi 17 au zaidi; bila kusahau the most important,
discrete graphics GPU.
5. Mtumiaji wa Nyumbani
Mtu yoyote ambaye hayupo kwenye vipengele nilivyovitaja hapo juu anafiti
hapa.Mtumiaji huyu huitaji desktop machine ambazo sio movable,Mashine hizi
hutengenezwa kwa asili ya kukaa sehemu moja, ile jikoni, sebuleni, chumbani,
etc.
Zile laptop za inchi 15 bado ni maarufu ingawa zile
za inchi 14 na 16 zinakuja juu siku hizi. Kila mtengenezaji wa PC hutofautiana
na mwingine na huzidiana kila mmoja katika sehemu tofauti. Usikimbilie kununua
mashine kubwa na kutumia hela nyingi.
Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 250GB au zaidi
kwenye Hard Disk; Display ya inchi 14-16; DVD burning optical drive (kwa asili
ya ku-burn CD).
hayo ndio ya kuzingatia uendapo kukunua PC. Kuwa
makini na kujua ni kundi lipi size yako.
Kwa maelezo Zaidi wasiliana kwa +255765327325
henrylameck@gmail.com
Shukran kwa ushauri
ReplyDeleteZingatia Haya Unapo Nunua Computer ~ Computer Services >>>>> Download Now
ReplyDelete>>>>> Download Full
Zingatia Haya Unapo Nunua Computer ~ Computer Services >>>>> Download LINK
>>>>> Download Now
Zingatia Haya Unapo Nunua Computer ~ Computer Services >>>>> Download Full
>>>>> Download LINK KM