umojannguvu.blogspot.com

Thursday 20 August 2015

Wafanyabiashara washauriwa kuanzisha viwanda vidogo





WAFANYABIASHARA ndogo mkoani hapa wametakiwa kutumia fursa zilizopo kuanzisha viwanda vidogo vya uzalishaji wa bidhaa badala ya kuwa wachuuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa alitoa rai hiyo jana alipowatembelea wafanyabiashara hao maarufu kama wamachinga, kwenye soko la Rehema Nchimbi Complex lililopo mjini hapa kwa lengo la kukagua mazingira ya kufanyia biashara sokoni hapo.

Galawa alisema biashara ya uchuuzi haiwaletei faida na mafanikio yanayohitajika badala yake inawafaidisha zaidi wazalishaji wenye viwanda, wengi wao kutoka nje ya nchi.

“Lazima mbadili mtazamo na kujikita katika kuanzisha viwanda vidogovidogo ili kuingia katika biashara ya uzalishaji bidhaa na usambazaji wake ambayo itawaletea mafanikio makubwa kiuchumi,” alisema.

Pia aliwataka wamachinga kujitathmini kila mmoja anavutiwa na kufanya uzalishaji wa bidhaa zipi huku wakichambua fursa zinazopatikana mkoani Dodoma.

Alizitaja baadhi ya fursa zilizopo mkoani Dodoma ni pamoja na uwepo wa viwanda vya nyama hivyo kuna nafasi nzuri ya kuanzisha viwanda vidogo vya kutengeneza bidhaa za ngozi kwa kuwa malighafi ya ngozi ya asili ya wanyama itapatikana kwa urahisi kutoka kwenye viwanda hivyo vya nyama.

Aliwahakikishia upatikanaji wa soko la bidhaa zao endapo watajitahidi kutengeneza bidhaa zenye ubora.

 


0 comments:

Post a Comment

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

CHAT BOX

Post zilizo tumwa

Recent Posts Widget

Tangaza Biashara yako mtandaoni

TANGAZA BIASHARA NAMI HAPA KWA BEI NAFUU KABISA

Unaweza kutangaza biashara yako sasa na hlmservice pia uta pata kujua mambo mengi ambayo mbali na biashara yako unaweza ukatengeneza pesa kwa namna moja ama nyingine kama jinsi nilivo elezea katika Makala za nyuma hapo

Wafanya biashara wengi wanatumia mda mwingi namna gani ya kukuza biashara zao ,Ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unahitaji kuitangaza biashara yako ili kuwa na mtandao mkubwa na wateja wako ,ni vyema ukatangaza biashara yako katika mitandao ili bidhaa zako zijulikane kwa haraka na upesi .

Pia wewe mfanya biashara ukiitaji kuwa na blog yako wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini , bei ni nafuu kabisa

Pia ukiitaji kuitangaza biashara yako kupitia blog yangu bei ni ndogo kabisa huu ni wakati wako wewe mfanya biashara

+255758061575 & +255684860817

henrylameck@gmail.com

henrylameck90@yahoo.com

Tukuyu Tour & Safari

Vadacom Ni Zaidi

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Kilimo Kwanza

Hlm servise

Latest movie

Movies

Computer books

Computer books