umojannguvu.blogspot.com

Friday, 21 August 2015

Kikundi kilichomlinda Lowassa matatani





POLISI mkoani Mbeya imetangaza kuchukua hatua dhidi ya kikundi kilichojifanya askari wa ulinzi kwenye msafara wa mgombea wa urais kupitia tiketi ya Chadema, Edward Lowassa alipowasili mkoani hapa.

Lowassa aliwasili mkoani hapa Agosti 14 mwaka huu, akiwa ameongozana na viongozi wa vyama vya siasa vinavyounda Ukawa kwa lengo la kumtambulisha na kuomba udhamini kwa wafuasi wa vyama hivyo kupeperusha bendera ya Chadema kugombea urais.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema katika msafara wake kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, kulionekana gari moja aina ya Landcruiser Pick up, nyeusi ambalo ndani yake kulikuwa na vijana waliovaa mavazi meusi,kofia aina ya Bereti nyeusi na nyekundu na miwani myeusi.

Kamanda Msangi alisema watu hao walikuwa na mwonekano kama askari na shughuli waliyoifanya ilikuwa ni kuongoza msafara, ulinzi na kazi nyingine zinazofanywa na polisi. Alisema kutokana na mwonekano wao na shughuli walizokuwa wakizifanya, walitafsiriwa kuwa ni jeshi lifanyalo kazi hizo, ambalo halikuwa likifahamika.

Alisema kutokana na sintofahamu hiyo, wananchi wengi walikuwa wakihoji ni jeshi gani. Alisema zilitumwa picha kwa njia ya Whatsapp kuonesha wasiwasi dhidi ya kikundi hicho. Alisema kutokana na hali hiyo, ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya, ilifungua jalada la uchunguzi kuwapata vijana hao kwa lengo la kuwahoji .

Kwa mujibu wa Kamanda, upelelezi ukikamilika, jalada litapelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ufafanuzi wa kisheria na hiyo ni kutokana na kuibuka kwa makundi ya aina hiyo, hasa kwa vyama vikubwa vya siasa hapa nchini.

“Katika kufanya ufuatiliaji huo, wapo watu wawili walikamatwa alfajiri ya Agosti 18 kwa mahojiano na baada ya maelezo yao kuchukuliwa walipewa dhamana,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

CHAT BOX

Post zilizo tumwa

Recent Posts Widget

Tangaza Biashara yako mtandaoni

TANGAZA BIASHARA NAMI HAPA KWA BEI NAFUU KABISA

Unaweza kutangaza biashara yako sasa na hlmservice pia uta pata kujua mambo mengi ambayo mbali na biashara yako unaweza ukatengeneza pesa kwa namna moja ama nyingine kama jinsi nilivo elezea katika Makala za nyuma hapo

Wafanya biashara wengi wanatumia mda mwingi namna gani ya kukuza biashara zao ,Ili uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unahitaji kuitangaza biashara yako ili kuwa na mtandao mkubwa na wateja wako ,ni vyema ukatangaza biashara yako katika mitandao ili bidhaa zako zijulikane kwa haraka na upesi .

Pia wewe mfanya biashara ukiitaji kuwa na blog yako wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini , bei ni nafuu kabisa

Pia ukiitaji kuitangaza biashara yako kupitia blog yangu bei ni ndogo kabisa huu ni wakati wako wewe mfanya biashara

+255758061575 & +255684860817

henrylameck@gmail.com

henrylameck90@yahoo.com

Tukuyu Tour & Safari

Vadacom Ni Zaidi

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Tembelea g2g.fm upate movie Kali

Kilimo Kwanza

Hlm servise

Latest movie

Movies

Computer books

Computer books